Cookies on Plantwise Knowledge Bank

Like most websites we use cookies. This is to ensure that we give you the best experience possible.

 

Continuing to use www.plantwise.org/KnowledgeBank means you agree to our use of cookies. If you would like to, you can learn more about the cookies we use.

Plantwise Knowledge Bank

Your search results

Plantwise Factsheets for Farmers

Matumizi salama ya salfa kudhibiti ubwiri kwenye mikorosho

Oidium anacardii
Tanzania

Tambua tatizo

Ubwiri unga ni ugonjwa wa kuvu unaoshambulia majani machanga, maua na matunda ya korosho. Ugonjwa huu usipodhibitiwa unaweza kupunguza mavuno kwa zaidi ya asilimia 80.
Vumbi la rangi ya kijivu au jeupe huonekana juu ya majani machanga, maua na matunda yaliyoshambuliwa.  Majani yaliyoshambuliwa sana hujikunjakunja na hatimaye huanguka.  Maua yaliyoshambuliwa hushindwa kuzaa matunda.  Matunda machache yanayozaliwa  hudumaa, hupasuka, huoza na huanguka yakiwa machanga.

Habari tangulizi

Ugonjwa wa Ubwiri unga huonekana zaidi wakati wa ukame na hupungua kipindi cha mvua.  Vimelea vya ugonjwa huu hujificha kwenye majani ya machipukizi machanga yaliyobanana na huweza kusambazwa kwa njia ya upepo kutoka msimu mmoja hadi mwingine.

Usimamizi

  • Ugonjwa huu huweza kudhibitiwa kwa kutumia aina nyingi za kemikali lakini Salfa ya unga hutumika zaidi kwa sababu ina madhara madogo kwa mtumiaji.
  • Salfa hupulizwa baada ya kuona asilimia tano ya miti yote ya korosho imeshambuliwa.
  • Salfa hujazwa kwenye tenki la bomba la kupulizia kwa ujazo unaoshauriwa.
  • Wakati unaofaa kupulizia ni kuanzia saa 12.00-3.00 asubuhi kwani umande uliopo kwenye majani husaidia Salfa inase.
  • Kiwango cha upuliziaji ni robo kilo (1/4) kwa mti sawa na kilo 87.5 kwa hekta kwa msimu.
  • Kwa msimu, Salfa hupulizwa mara tano (5) kila baada ya siku 14, lakini mpulizo wa mwisho  ambao ni wa tano hupulizwa baada ya siku 21.
  • Mpuliziaji anashauriwa kupulizia Salfa sambamba na upepo unakoelekea ili  isimrudie na kumdhuru.
Daraja la 1 la viwatilifu kulingana na shirika la Afya Duniani (WHO) (na bidhaa yenye kibandiko chekundu kwaTanzania) hazishauriwi kutumika. Daraja la II la viwatilifu kulingana na WHO (na bidhaa yenye kibandiko cha njano-Tanzania), (hazishauriwi Tanzania kutokana na Mpango wa Udhibiti Husishi wa Visumbufu vya Mimea).  WHO hupendelea daraja la 3 au U, na Tanzania inashauri bidhaa zenye  kibandiko cha kijani au bluu. Kagua na zingatia kutumia Viwatilifu vilivyosajiliwa na (MAFC / TPRI).

Wakati wa kutumia kemikali, vaa mavazi ya kinga wakati wote na ufuate maelekezo kwenye lebo ya bidhaa, kama vile kipimo, majira ya kuweka, muda kabla ya kuvuna

Mapendekezo katika vidokezo hivi yanatumika katika: Tanzania

WAANDISHI: Jubilant Mwangi, Costantine P. Mboya, Caroline S. Swai
Plantwise
©CAB International. Published under a CC-BY-SA 4.0 licence.

Plantwise Factsheets Library app

Get all of the factsheets and pest management decision guides from this website in an offline format via the Plantwise Factsheets Library app.