Cookies on Plantwise Knowledge Bank

Like most websites we use cookies. This is to ensure that we give you the best experience possible.

 

Continuing to use www.plantwise.org/KnowledgeBank means you agree to our use of cookies. If you would like to, you can learn more about the cookies we use.

Plantwise Knowledge Bank

Your search results

Plantwise Factsheets for Farmers

Mnyauko bakteria kwenye nyanya

Ralstonia solanacearum
Tanzania

Tambua tatizo

Bakteria mnyauko ni ugonjwa unaoweza kujitokeza katika hatua zote za ukuaji wa mmea. Kwanza unajionyesha kwa kunyauka kwa majani ya machanga, baadaya siku mbili au tatu mmea wote hunyauka haraka bila majani kubadilika na kuwa ya njano. Shina la mmea ulioathirika hubadilika na kuwa na rangi ya kahawia. Shina la mmea ulioathirika likikatwa na kulowekwa kwenye glasi ya maji ndani ya dakika moja ,linatoa utomvi mfano wa maziwa kuonyesha kwamba bacteria wanatoka.

Habari tangulizi

Mnyauko bacteria ni ugonjwa unaopatikana kwenye udongo na unaathiri mimea kupitia kwenye mizizi au shina. Vilevile hambukizwa kupitia sehemu ya mmea yenye jeraha lililosababishwa na vifaa vya kilimo au minyoo fundo. Pia huishi kwenye mazao ya familia moja na nyanya kama blinganya. Husambaa vilevile kwa rijia ya maji ya umwagiliagi na mbegu. Ni rahisi kuzuia / kakinga kuliko kutibu.

Usimamizi

  • Tumia aina ya mimea inayostahimili ugonjwa (Fortune Maker, Kentom, Taiwan F1).
  • Usioteshe nyanya maeneo ya bondeni ambayo daima ni maji maji na yenye historia ya mnyauko bacteria
  • Fanya mzunguko wa nyanya na mazao mengine yasiyo ya jamii ya nyanya kama vile nafaka, kunde, miwa, kabichi na siyo pilipili wala viazi mviringo
  • Epuka kuhamisha vifaa/vyombo/maji kutoka eneo lenye ugonjwa kwenda eneo lisilo na ugonjwa.
  • Simika miti wiki mbili baada ya kupandikiza miche na punguza majani ili kuipa mimea hewa.(angamiza vijidudu kwenye visu vilivyotumika kwa kutumia blichi kabla ya kutumia kwenye mmea mwingine).
  • Epuka umwagiliaji wa kutumia mifereji kwa kuwa hueneza ugonjwa huu ulio kwenye udongo haraka zaidi. (kama unatumia mfereji, anza kumwagilia eneo jipya kuelekea lile la zamani).
Endapo utagundua mmea mmoja umeathirika katika shamba lako chukua hatua ya kututhibiti ugonjwa.
  • Ng’oa mmea, mizizi na udongo wa eneo hilo na kuchoma vyote, usivibebe vikiwa wazi kwenye shamba kwani vitaeneza ugonjwa, usioteshe tena nyanya kwenye shimo hilo.
  • Unaweza kupunguza mashambulizi kwa kunyunyiza sumu aina ya copper oxychloride au copper hydroxide, zote ni sumu hatari (daraja la II WHO). Vaa vifaa vya kujikinga.nyunyiza dawa siku 14 kabla ya kuvuna.

Wakati wa kutumia kemikali, vaa mavazi ya kinga wakati wote na ufuate maelekezo kwenye lebo ya bidhaa, kama vile kipimo, majira ya kuweka, muda kabla ya kuvuna

Mapendekezo katika vidokezo hivi yanatumika katika: Tanzania

WAANDISHI: Adeltruda Massawe, Irene Kessy, Livin K. Mahoo, Mansuet Tilya, Martin Kimani, Richard Musebe
Horti Tengeru, Tanzania
©CAB International. Published under a CC-BY-SA 4.0 licence.

Plantwise Factsheets Library app

Get all of the factsheets and pest management decision guides from this website in an offline format via the Plantwise Factsheets Library app.