Cookies on Plantwise Knowledge Bank

Like most websites we use cookies. This is to ensure that we give you the best experience possible.

 

Continuing to use www.plantwise.org/KnowledgeBank means you agree to our use of cookies. If you would like to, you can learn more about the cookies we use.

Plantwise Knowledge Bank

Your search results

Kiongozi cha Usimamizi wa Wadudu: Orodha njani na njano

White flies on tomatoes

Bemisia tabaci Swahili: Inzi weupe
Kenya
 • Tumia karatasi nyeupe au nyeusi za plastiki kama matandazo,siku 10 hadi 20 baada ya kupandikiza miche ili kuwavutia na kuwaua nzi weupe.
 • Tumia matandazo ya kawaida (majani yaliyokauka) baada ya kupandikiza mimea itakayokuwa ikinyunyiziwa maji.
 • Tumia neti za kuweka kivuli zenye mashimo madogo sana au handaki kwa wiki 3 hadi 5 wakati miche ingali katika vitangu, ili kuzuia nzi weupe kuivamia.
 • Hifadhi maadui wa kawaida wa nzi weupe (kwa mfano nyigu,mdudu kibibi) kwa kuweka matandazo au ua la miti yenye maua iliyooteshwa kandokando mwa shamba ili kuwapa makao.(kwa mfano Tithonia, Lantana)
 • Pandikiza miche muda mfupi baada ya au wakati wa msimu wa mvua.
 • Panda mimea inayozuia au kuwafukuza nzi weupe kama vile mgiligilani na bangi ya shambani (Mexican Marigold) kila baada ya mistari mitatu au minne ya minyanya.
 • Panda mimea kwa mfano tumbaku,maharagwe na mahindi, ambayo ina uwezo ya kuwavutia nzi weupe kando kando mwa shamba,ambapo wadudu hawa wanaweza kudhibitiwa na kemikali.
 • Weka shamba lako bila magugu wakati mimea inapoendelea kukua, kwa kuwa nzi weupe pia hupenda kuishi kwenye hayo magugu.
 • Chunguza na utafute:
  • Mayai yaliyo meupe au rangi ya maji ya kunde na nzi weupe waliokomaa upande wa chini wa matawi machanga.
  • Wingu la nzi weupe watatu hadi watano wanaotua kwenye matawi baada ya mmea kutikiswa.
  • Ubadilikaji wa rangi ya sehemu ya juu ya matawi na kuwa rangi ya manjano.
  • Anzisha hatua za kudhibiti wakati nzi weupe watatu wanapopatikana au kuonekana baada ya mmea kutikiswa.
 • Tumia mitego yenye ute na yenye rangi ya manjano ili kuwanasa nzi weupe waliopevuka. Tumia mitego minne kwa kila eneo la mita 300.
 • Nyunyiza viuwa wadudu vyenye 'Azadirachtin 0.03%,siku kumi na tano baada ya kupandikiza, kwa kipimo cha mililita 50 kwa lita 20 za maji.
 • Tumia sabuni ya maji kwa kunyunyiza, tumia kipimo cha vijiko vitatu vya chakula kwa lita moja ya maji.
 • Nyunyiza mchanganyiko wa pilipili moto uliotayarishwa kwa kukatakata pilipili 30, halafu kuloweka kwa maji moto ya lita moja,kwa muda wa siku moja; baadae mchanganyiko huo huwekwa kwenye lita 10 za maji, pia ongeza vitone 20 vya sabuni ya maji kabla ya kutumia huu mchanganyiko.
 • Nyunyiza maadui wa nzi weupe kwenye minyanya yako, kwa mfano nyigu aina ya Encarsia formosa na pia kutumia kuvu wanaokula wadudu kama vile Beauveria bassiana,na Lecanicillium lecanii
 • Vaa nguo za kujikinga kutokana na kemikali na ufuatilie maagizo yaliyo kwenye chupa au pakiti.
 • Nyunyiza wakati wa asubuhi na mapema au baadae jioni, ili usidhuru nyuki.
 • Tupa pakiti au chupa za viuwa wadudu kwa njia inayofaa, ili kuzuia kudhuru viumbe vya majini.
 • Badilisha viuwa wadudu vyenye dawa aina tofauti tofauti ili kuzuia wadudu kuwa sugu
 • Lowa mimea na viuwa wadudu vyenye 'imidacloprid' kwa kipimo cha miligramu 5 kwa lita 20 za maji. Dawa hii ni aina iitwayo 'Neonicotinoid, imeorodheshwa kwenye IRAC 4A. Inafanyakazi kwa kuingia kwenye matawi, au wakati inapoguswa au ni sumu inapoliwa na viwavi.
 • Daraja la pili la shirika la afia duniani (Ina hatari wastani au kiasi), PHI Siku tatu, kiwango kinachobaki kwa mimea ni 0.5.
 • Nyunyiza viuwa wadudu vyenye 'lambda-cyhalothrin' kwa kipimo cha mililita 7 kwa lita 20 za maji. Kanuni ya tatu ya IRAC
 • Daraja la pili la shirika la afia duniani (Ina hatari wastani au kiasi), PHI Siku tatu, kiwango kinachobaki kwa mimea ni 0.01.
 • Nyunyiza viuwa wadudu vyenye 'alpha-cypermethrin' 10EC kwa kipimo cha mililita 5 kwa kila lita 20 za maji. Kanuni ya tatu ya IRAC
 • Daraja la pili la shirika la afia duniani (Ina hatari wastani au kiasi), PHI Siku tatu, kiwango kinachobaki kwa mimea ni 0.2.
Waandishi: Stephen Kiritai (MOALF), Miriam Otipa (KALRO), K. Kagai (MOALF), Benson Ngigi (MOALF), Margaret Mulaa (CABI), Paul Kiige (MOALF)and Judith Oyoo (KALRO)

CREATED/UPDATED: August 2014
PRODUCED BY: Plantwise

©CAB International. Published under a CC-BY-SA 4.0 licence.