Cookies on Plantwise Knowledge Bank

Like most websites we use cookies. This is to ensure that we give you the best experience possible.

 

Continuing to use www.plantwise.org/KnowledgeBank means you agree to our use of cookies. If you would like to, you can learn more about the cookies we use.

Plantwise Knowledge Bank

Your search results

Kiongozi cha Usimamizi wa Wadudu: Orodha njani na njano

Tuta absoluta (tomato leaf miner) on Tomato

Tuta absoluta
Kenya
 • Panda miche iliyosafi na haijaathirika na viwavi aina ya Tomato leaf miner.
 • Pangilia minyanya na mimea mingine kama vile mahindi, maharagwe na kabeji.
 • Chimbua na uchome mimea yote iliyoathirika pamoja na magugu kama mtunguja mwitu.
 • Safisha vifaa vyote vinavyotumika kwa usafirishaji wa nyanya kama vile masanduku,matenga na hata malori kwa kutumia sabuni na maji.
 • Chunguza na utafute:
  • Nondo wenye mchanganyiko wa rangi ya maji ya kunde na ya fedha.
  • Mashimo meupe au krimu yaliyoshikana na yanayooza, upande wa juu na chini wa matawi.
  • Viwavi vyenye rangi ya kijani kibichi na wenye vichwa vyeusi ndani ya mashimo.
  • Utandu wa hariri uliotengenezwa na viwavi, ili kukunja matawi kulinda viwavi wengine wachanga wanaoota.
  • Matawi yaliyobadilika rangi au kuoza kwa kuathirika na viwavi.
  • Alama za kutobolewa upande wa juu wa matunda, pia kwenye shina la mmea na kovu leusi lililokauka kwenye shimo alilotoka kiwavi.
 • Chukua hatua za dharura kudhibiti wakati unapoona kiwavi kimoja hadi vitatu kila wiki.
 • Tumia mikono kuvyoga viwavi wkati unapoona ishara za uchimbaji wa mashimo.
 • Unaweza kuwanasa kwa wingi kutumia maji yaliyo na kemikali za kuwavutia (kwa mfano Pherodis kwa kiwango cha pakiti 4 kwa ekari, inauzwa na kampuni kama vile Koppert Biological Systems Kenya, na Tutrack ipatikanayo pale Kenya Biologics.
 • Zika matawi na matunda yote yaliyoathirika kwenye shimo lenye urefu wa sentimita 50 hadi 100.
 • Unaweza pia kutimia mitego nyeusi yenye ute wa kuwanasa, hizi huwekwa sentimita 15 hadi 20 juu ya ardhi ili kuwashika wadudu waliokomaa (tumia vipande 24 kwa kila ekari, inauzwa na kampuni ya Koppert Biological Systems)
 • Tumia neti za kuzuia wadudu kwenye paa na kando kando mwa nyumba aina za 'greenhouse', ili kuzuia uhamaji kwa wadudu kutoka eneo moja hadi lingine.
 • Tumia nguo maalum za kujikinga, kila wakati unapotumia viuwa wadudu au dawa shambani.
 • Fuata maagizo yaliyokwenye pakiti au chupa ya viuwa wadudu, kwa mfano kiwango cha kutumia, wakati wakuinyunyizia mimea, muda kabla ya kuvuna, idadi ya wakati mimea inafaa kunyunyiziwa na muda kabla ya kurudi kwenye shamba lilonyunyiziwa. Usimwage viuwa wadudu kwenye mirizabu au michirizi.
 • Viuwa wadudu vilivyo orodheshwa kwenye daraja la pili la Shirika la afia duniani vinaweza kutoruhusiwa katika mipangilio ya kuzuia wadudu katika sehemu unayokaa.
 • Kila mara fuatilia ushauri wa orodha ya viuwa wadudu vilivyosajiliwa hivi karibuni (PCPB)
 • Tumia: viuwa wadudu vyenye 'Spinetoram'(Kwa mfano Radiant 120 SC, kwa kipimo cha mililita 180 hadi 300 kwa ekari moja au mililita 18 hadi 30 kwa lita 20 za maji).
 • Daraja la tatu la shirika la afia duniani, Mstari wa rangi ya samawati (Ina hatari wastani au kiasi), PHI Siku tatu.
 • Tumia: viuwa wadudu vyenye 'Chlorantraniliprole'(Kwa mfano Coragen 20 SC, kwa kipimo cha mililita 5 kwa lita 20 za maji)
 • Daraja la U la Shirika la afia duniani, Mstari wa rangi ya kijani kibichi (Ikitumika vizuri haiwezi kuwa na madhara yeyote), kiwango kinachobaki kwenye mimea ni miligramu 0.05 kwa kilo moja ya mimea, PHI Siku tatu.
 • Tumia: viuwa wadudu vyenye 'Flubendiamide' (Kwa mfano Belt 480 SC, kwa kipimo cha mililita 4 kwa lita 20 za maji.)
 • Daraja la pili la shirika la afia duniani, Mstari wa rangi ya manjano, (Ina hatari wastani au kiasi), PHI Siku tatu
Waandishi: Miriam Otipa (KALRO), Paul Kiige (MOALF), Eunice Ringera (KEPHIS), Philip Wendot (UON) and Benson Masinde (MOA), Peninah Munyao (MOALF), Judith Oyoo (KALRO), Wilson Nabakwe (MOALF)

CREATED/UPDATED: August 2014
PRODUCED BY: Plantwise

©CAB International. Published under a CC-BY-SA 4.0 licence.