Cookies on Plantwise Knowledge Bank

Like most websites we use cookies. This is to ensure that we give you the best experience possible.

 

Continuing to use www.plantwise.org/KnowledgeBank means you agree to our use of cookies. If you would like to, you can learn more about the cookies we use.

Plantwise Knowledge Bank

Your search results

Kiongozi cha Usimamizi wa Wadudu: Orodha njani na njano

Leaf miner on tomato

Liriomyza trifolii Viwavi aina ya Leafminer
Kenya
 • Kuwa na mazoea ya kupangilia nyanya na mimea mingine wasioipenda viwavi aina ya leaf miner, kama vile mahindi, mtama au mwimbi.
 • Hifadhi maadui wa kawaida kama vile nyigu na bunzi au mdudu kibibi kwa kupanda nyua za maua kingoni mwa shamba.
 • Toa mabaki yote ya mimea, ili kuzua viwavi hawa kuzaliana humo.
 • Panda ua la kibaazi au Tephrosia kuzunguka shamba lako ili kuwafukuza viwavi aina ya Leafminer mbali na mimea yako.
 • Weka matawi yaliyokauka shinani mwa mimea ili kuzuia pupa wasiingie kwenye mchanga na kuota au kupevuka.
 • Tafuta nzi wadogo wenye rangi ya manjano na nyeusi, waaopepea juu ya mimea.
 • Tumia mitego yenye rangi ya manjano ili kunasa nzi waliopevuka.
 • Chunguza miche iliyo kwenye vitangu na utafute mashimo na alama za mayai yaliotagwa, kabla ya kuipandikiza kwenye shamba.
 • Kwenye matawi tafuta alama nyeupe za kutobolewa, kubadili kwa rangi ya manjano na mashimo yaliyosababishwa na nzi wa leafminer wanaotaga mayai kwenye matawi hayo.
 • Anza kudhibiti viwavi hivi vya Leafminer mara moja pale unapoona idadi yao imeongezeka na zaidi ya asilimia thelathini ya tawi limeathirika.
 • Ng'oa miche iliyoathirika kutoka kwenye vitangu, kwamua matawi yaliyoathirika na uyachome au uzike kwenye shimo lenye urefu wa mita moja.
 • Tumia beseni lenye rangi ya manjano na ulijaze nusu na maji au tumia mitego ya manjano ya kunasa ili kuwavutia na kuwaua nzi aina ya Leafminer
 • Nyunyizia viuwa wadudu vyenye asili ya miti kama muarubaini (kwa mfano Azadirachtin Neemark EC, Neemaj Super -3000 na Neemroc EC) katika viwango vilivoshauriwa.
 • Nyunyizia viuwa wadudu mapema asubuhi au baade jioni ili usiathiri nyuki
 • Soma na ufuatilie maagizo kwenye pakiti au chupa.
 • Tupa pakiti au chupa za viuwa wadudu kwa njia inayofaa, ili usiathiri samaki na wanyama wengine wa maji.
 • Nyunyizia dawa yenye 'abamectin' (mfano Abalone 18EC, Agrimec 18EC, gramu 20 kwa kilo za Amazing top pamoja na gramu themanini kwa kilo za Dynamec) kwa viwango vinavyostahili. Zinauwezo wa kuingia kwenye matawi. Hufanya kazi wakati viwavi wanapoigusa au kuila na kuingia tumboni mwao. IRAC 6
 • Daraja la pili la shirika la afia duniani:(Ina hatari wastani au kiasi), PHI siku saba.
 • Nyunyiza dawa zenye bifethrin kwa kiwango cha mililita 5 katika lita ishirini za maji. Hufanya kazi wakati viwavi wanapoigusa au kuila na kuingia tumboni mwao; IRAC 3A
 • Daraja la pili la shirika la afia duniani:(Ina hatari wastani au kiasi), PHI siku tatu. Kiwango kinachobaki kwenye mimea ni 0.2.
 • Lowa mimea na dawa yenye imidaclorid kwa viwango vilivyopendekezwa. Dawa hizi ni za aina ya Neonicotinoid na hufanya kazi kwa kuingia kwenye matawi; wakati viwavi wanapoigusa na wanapoila na kuingia tumboni mwao.IRAC 4A
 • Daraja la pili la shirika la afia duniani:(Ina hatari wastani au kiasi)
Waandishi: Miriam Otipa (KALRO), Stephen Kiritai, K. Kagai and Benson Ngigi (MOALF), Wilson Nabakwe (MOALF), Peninah Munyao (MOALF) and Judith Oyoo (KALRO)

CREATED/UPDATED: August 2014
PRODUCED BY: Plantwise

©CAB International. Published under a CC-BY-SA 4.0 licence.