Cookies on Plantwise Knowledge Bank

Like most websites we use cookies. This is to ensure that we give you the best experience possible.

 

Continuing to use www.plantwise.org/KnowledgeBank means you agree to our use of cookies. If you would like to, you can learn more about the cookies we use.

Plantwise Knowledge Bank

Your search results

Plantwise Factsheets for Farmers

Udhibiti wa “Maize Lethal Necrosis” kwa kungoa mahindi

Maize lethal necrosis disease
Tanzania

Tambua tatizo

“Maize Lethal Necrosis” ni ugonjwa hatari unaouwa mahindi ambao husababishwa na virusi vya aina mbili. Dalili za ugonjwa katika hatua za awali ni michirizi mirefu ya njano kwenye majani inayofanana na  ugonjwa wa milia wa mahindi lakini mistari iliyopo “maize lethal necrosis” hutanuka kutokea pembezoni mwa jani kuelekea kwenye shina. Ugonjwa wa “angular leaf spot” pia unaozesha na kukausha majani lakini tofauti yake ni kwamba hali hii hutokea kama madoa madogo madogo kwenye majani. Dalili nyinginezo ni majani kujikunja, kudumaa kwa mmea na kuzeeka mapema hatimaye kufa; Mimea iliyokufaa huonekana ndani ya shamba katikati ya mimea yenye afya; maambukizi ya ugonjwa wakati mhindi unakaribia kubeba ni mbelewele kukosa shamvua, na bumzi kuweka mbegu chache.

Habari tangulizi

Ugonjwa wa “Maize Lethal Necrosis Disease” huzidi wakati wa ukame ambapo hakuna unyevunyevu kwenye udongo. Mvua nyingi husababisha tatizo la ugonjwa kupungua. Hivyo ni vyema mahindi yakapandwa mapema wakati wa msimu wa mvua za masika na mazao mengine yakapandwa msimu wa mvua fupi za vuli.  Inashauriwa kungoa mimea iliyoathirika ili kuondoa chanzo cha ugonjwa shambani kwa kuwa virusi vya  ugonjwa husambazwa na vithiripi, vidukari na panzi kutoka mimea iliyoathirika kwenda kwenye mimea isiyoathirika. Virusi hivi havipatikani kwenye udongo. Mbegu kinzani dhidi ya ugonjwa huu hazipatikani Afrika ya Mashariki.

Usimamizi

  • Kagua shamba mara kwa mara katua hatua zote za ukuaji wa mahindi ili kutambua mimea yenye dalili za kuathirika mapema.
  • Ngoa mimea yote yenye dalili za kuathirika na usiache kwa kuwa mimea iliyoathirika haitaweza kuzaa
  • Kusanya mimea uliyongoa bila udongo na kutoa nje ya shamba ili  jua likaushe na kupoteza ugojwa halafu choma moto.
  • Njia hii ya udhibiti  inaleta matokea  mema  inapotumika pamoja  na unyunyuziaji wa viuatilifu kuuwa wadudu wasambazao ugonjwa pamoja na kupanda kwa wakati.

Wakati wa kutumia kemikali, vaa mavazi ya kinga wakati wote na ufuate maelekezo kwenye lebo ya bidhaa, kama vile kipimo, majira ya kuweka, muda kabla ya kuvuna

Mapendekezo katika vidokezo hivi yanatumika katika: Kenya, Tanzania

WAANDISHI: Jubilant Mwangi, Rebecca Mawishe, Esther Chacha
Plantwise

Plantwise Factsheets Library app

Get all of the factsheets and pest management decision guides from this website in an offline format via the Plantwise Factsheets Library app.